Thursday, June 21, 2012

DIAMOND KUPAMBA MISS DAR INTERCOLLEGE 2012



Shindano la kumsaka mrembo atake wakilisha vyuo vikuu katika shindano la Miss Tanzania linatrajiwa kufanyika June 22 mwaka huu. Shindano hilo ambalo awali lilitakiwa lifanyike june 8 ila lilishindwa kufanyika kutokana na baadhi ya washiriki kua katika mitihani.Shindano hilo linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa makumbusho ya taifa ambayo yanatizamana na chuo cha usimamizi wa fedha IFM. Warembo kutoka vyuo mbalimbali jijini Dar es salaam watachuana kuwania umalkia huo wa vyuo vikuu, Vyuo vinavyotarajiwa kushiriki katika shindano hilo ni CBE,IFM.OUT, DSJ, Ustawi wa jamii n.k.Baadhi ya warembo waliosibitisha kushiriki ni Veronica Ngota, Rose Muchungusu, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Jacquiline Cliff, Neema Michael, Veronica Yola, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja, Jamila Hassan n.k  Taji la Miss dar entercollege linashikiliwa na Rose Msuya wa IFM.
Wadhamini katika shindano hilo ni TBL Kupitit kinywaji cha REDDS, Dodoma wine, Ndege insurance, Grand villa hotel, Clouds fm n.k
Shindano hilo litapabwa na shoo kali kutoka kwa the ladies finest Diamond Platinumz