Friday, June 21, 2013

KIJANA AGAINST AIDS CAMPAIGN

Chuolife organization ikishirikiana na wadau mbalimbali wa UKIMWI wanakuletea kampeni yenye kuhamasisha vijana kujiepusha na vitendo vitakavopelekea kupata maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI. Kampeni hii itazunguka katika vyuo vyote vya jijini dar es salaam na Morogoro. Kampeni hii inayokwenda kwa jina la KIJANA AGAINST AIDS ina lengo la kupunguza maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI kwa vijana walioko na wasiokua vyuoni. Chuolife inaomba ushirikiano wako wewe kijana katika kufanikisha kampeni katika chuo chako.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kampeni hii wasiliana na mratibu Mathayo Francis 0714 501 141