Kinyang'ayiro cha kumsaka miss lake zone intercolleges 2012
kinatarajiwa kufanyika june 23 mwaka huu mjini Bukoba katika katika ukumbi wa
linaz club. Katika shindano hilo ambalo litashereheshwa na mchekeshaji maarufu
kama mpoki (Bepari la kihaya), na kuburudishwa na mwanamama malkia wa taarabu
nchini ambaye pia ni mshindi wa tuzo za KTMA 2012 Khadija Kopa litawashilikisha
warembo kutoka vyuo vilivyopo kanda ya ziwa. Warembo 15 watachuana kugombea
umalkia wa vyuo kanda ya ziwa, vyuo vitavyotoa warembo katika shindano hilo ni
CBE, SAUT, Tumaini n Utalii kutoka Mwanza, Open university na SAUT kutoka
Kagera na pia watashiriki warembo kutoka Shinyanga. Shindano hilo limedhaminiwa
na TBL Kupiti kinywaji chake cha REDDS, Bukoba wadau blogspot, Kasibante FM, Bukoba
cable TV, Smart hotel na Kiloyera tours.