Friday, June 8, 2012
SHERIA YA MAVAZI CBE YAZOELEKA
Wanafunzi wanaosoma chuo cha elimu ya biashara CBE wamesema sheria ya mavazi iliyowekwa mwanzoni mwa mwaka huu chuoni hapo wameshaizoea hivyo aiwasumbui tena. Wakiongea kwa nyakati tofauti wanafunzi wa chuo hicho, "mwanzo ilikua ngumu sana kwetu kuzoea ila kwa sasa tunaona kawaida hivyo aitusumbui' Alisema mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani. Sheria ya mavazi iliwekwa chuoni hapo mwanzoni mwa mwaka huu kudhibiti mavazi ambayo hayazingatii maadili ya kitanzaniaila ilipokelewa kwa hisia tofauti na wanafunzi wa chuo hicho.Wapo ambao waliiona ni sahihi na wapo walioiona kua ni kuingilia maisha ya mtu.